Wasiwasi umezidi kuhusu hatiamya chombo cha anga za juu cha mataifa ya Ulaya ambacho kilikuwa safarini kwenda sayari ya Mars, na ambacho kilitarajiwa kutua kwenye sayari hiyo Jumatano.
Wasiwasi umezidi kuhusu hatiamya chombo cha anga za juu cha mataifa ya Ulaya ambacho kilikuwa safarini kwenda sayari ya Mars, na ambacho kilitarajiwa kutua kwenye sayari hiyo Jumatano.
Hii ni baada ya mawasiliano na chombo hicho kukatika.
Wataalamu wanasema mawasiliano na roboti iliyo kwenye chombo hicho cha Schiaparelli yalikatika chini ya dakika moja kabla ya wakati ambao chombo hicho kilitarajiwa kutua katika sayari hiyo.
Setilaiti zinazoizunguka sayari ya Mars zimejaribu kufanya uchunguzi kubaini hatima ya chombo hicho kilichojaribu kutua, bila mafanikio.
Chombo hicho kilikuwa na muda wa chini ya dakika sita kupunguza kasi yake ya kilomita 21,000 kwa saa kiasi cha kukiwezesha kutua salama kwenye sayari hiyo.
- Chombo cha anga za juu cha Ulaya kutua Mars
- Mpango wa Marekani kupeleka watu Mars
- Wana anga wawili wa China wafika anga za juu
Moja ya setilaiti za Marekani zilijaribu kuwasiliana na Schiaparelli lakini hakuna majibu yaliyopatikana.
Kuna wasiwasi kwamba roboti hiyo ilianguka vibaya kwenye sayari hiyo na kuharibika.
Shirika la Anga za Juu la Ulaya hata hivyo bado linasema ni mapema sana na linaendelea kuwa na matumaini.
Wahandisi na wataalamu wengine watajaribu kufanya uchunguzi, sana kwenye mifumo yao ya kompyuta, kubaini ni kwa nini mawasiliano yalikatika na kisha wajaribu kuyarejesha.
Shughuli hii yote inaweza kuchukua siku kadha.
Post a Comment