Header Ads

FAHAMU UGONJWA WA PELVIC INFAMMATORY (PID) NA JINSI YA KUJIKINGA

FAHAMU UGONJWA WA PELVIC INFAMMATORY (PID) NA JINSI YA KUJIKINGA

Pelvic Inflammatory Disease PID
Pelvic inflammatory disease,  ugonjwa huu unafahamika kama  PID, ni maambukizi kwenye via vya uzazi wa mwanamke . PID ni miongoni kwa magonjwa hatari sana kwa mwanamke una madhara makubwa na unaambukizwa kwa njia ya kujamiiana. 
Ugonjwa huu unaweza ukapelekea uharibifu mkubwa kwenye mfuko wa uzazi,mayai ,mirija ya uzazi au sehemu nyingine za uzazi wa mwanamke
 Na pia Pid ni moja ya chanzo cha ugumba kwa mwanamke ambacho kinaweza kuzuilika.

TAKWIMU ZINAONESHA
Kila mwaka,zaidi ya wanawake milioni moja nchini marekani wanapatwa na ugonjwa huu wa PID,
Matokeo yake zaidi ya wanawake 100000 wanakuwa wagumba  kila mwaka.
Zaidi ya hayo  idadi kubwa ya mimba zaidi ya 100000 inatungiwa kwenye mirija ya uzazi(ectopic pregnancy) inahusishwa na tatizo hilo la PID. 
Kiwango kikubwa cha maambukizi  ni kwa wasichana wadogo

VISABABISHI VYA PID
Kwa kawaida  mlango wa uzazi (cervix) inazuia bakteria ambao wameingia ukeni wasisambae sehemu zingine za ndani za uzazi
Kama mlango wa uzazi cervix umepatwa na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana kama kisonono na/au clamydia
 Mlango huo wa uzazi cervix unaathirika na unakuwa na uwezo mdogo 
wa kuzuia kusambaa kwa bakteria sehemu za ndani za uzazi.
PID inatokea pale vimelea vya magonjwa vinaposafiri kutoka  kwenye mlango wa uzazi cervix kwenda sehemu za juu za uzazi.
Aslimia 90 ya PID husababishwa na   kutotibiwa ugonjwa wa kisonono na klamidia
Visababibishi vingine vya pid
👉Kutoa mimba
👉Kujifungua
👉Vipimo kwenye mlango wa uzazi

DALILI ZA PID
Dalili za PID zinatofautiana,zinaweza kuwa zifuatazo
👉Maumivu ya tumbo sehemu ya chini au upande wa kulia
👉Kutokwa kwa uchafu ukeni usio wa kawaida wenye rangi ya kijani au ya njano na wakati mwingine una harufu isiyo ya kawaida
👉Kichefuchefu na kutapika
👉Homa ya huu
👉Maumivu wakati wa tendo la ndoa
👉Maumivu wakati wa kukojoa
👉Maumivu sehemu ya kulia upande wa juu wa tumbo
MAMBO YANAYOWEZA KUMUWEKA HATARINI MWANAMKE KUPATA PID
Kuna baadhi ya vitu ambavyo vinamuweka mwanamke katika hatari ya 
kupata PID ni kama vifuatavyo
1.Wanawake wenye magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya kujamiiana kama kisonono na klaimidia wako hatarini sana kupata PID
2.Wanawake ambao waliwahi kupata PID wako hatarini kupata tena
3. Wasichana wadogo wapo hatarini kupata PID kuliko wazee.
4.Wanawake wenye wapenzi wengi wako katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa na PID
Baadhi ya tafiti zinaeleza uoshaji wa uke unachangia kupata PID.
.Kuosha uke( Douching) kunaweza pelekea  kusukuma bakteria sehemu za juu za via vya uzazi na kuzuia kutoka kwa uchafu ambao mwanamke angeweza kutumia kama ishara  ya kwenda kuonana na wataalamu wa Afya mapema
MADHARA YA PID
Kutokea /kujirudia kwa PID kunaweza kusababisha
kutokea kuharibika mirija ya uzazi ambayo inaweza kupelekea
👉Ugumba
👉Mimba kutunga kwenye mirija ya uzazi(ectopic pregnancy)
👉Maumivu makali kwenye shingo ya kizazi
Kati ya wanawake nane (8) wanaougua PID mmoja(1) unakuwa mgumba
JINSI YA KUJIKINGA NA PID 
PID inaweza kuzuilika kabisa ,kisababishi kikubwa cha pid ni magonjwa ya zinaa Mambo ya kuzingatia ili uweze kujikinga na PID 
👉Epuka kufanya mapenzi na watu wengi
👉Tumia njia za uzazi wa mpango(barrier) kama kondomu
👉Tumia spermicides kwa kila tendo la ndoa hata kama unameza  vidonge vya uzazi
👉 Usitumie  IUDs kama  unawapenzi wengi.
Note
IUDs ni vitu vinavyowekwa ndani ya uke kuzuia mimba
👉Wahi matibabu ukiona dalili zozote  za PID au za magonjwa ya zinaa kama kuto=
kwa na uchafu usio wa kawaida ukeni,maumivu kiunoni nk
👉Pia fanya uchunguzi wa afya ya uzazi mara kwa mara  ili kama kuna tatizo ligundulike na litibiwe kabla halijasambaa kwenda kwenye viungo vya ndani vya uzazi
MATIBABU YA PID
Antibiotics  hutumika kutibu PID kwa awali  na kwa matibabu ya PID ya awali antibiotics za kunywa hutumika.
Kama tatizo limekuwa kubwa mgonjwa atapewa antibiotics ya kunywa na pia ya sindano,kama utagundulika na tatizo hili mwenza wako au wenza wako watibiwe hata kama hawana dalili zozote vinginevyo tatizo litaweza kujirudia mtakaposhiriki tendo la ndoa
TATIZO LIKIZIDI LIKAWA KUBWA YANI  USAHA UKAVIMBIA ITAKUBIDI UFANYIWE UPASUAJ

No comments