Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC)
Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC), Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamini Mkapa Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amethibitisha hilo na kusema kuwa Rais Magufuli amemteua Prof. Lazaro S.P. Busagala kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki (TAEC) kuanzia tarehe 22 Machi, 2018.Kabla ya uteuzi huo Prof. Busagala alikuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) – Taaluma na Utafiti.
Lakini pia Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Damian Gabagambi kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kuanzia tarehe 22 Machi, 2018. Prof. Gabagambi anachukua nafasi ya Bw. Mlingi Elisha Mkucha ambaye atapangiwa kazi nyingine. Kabla ya uteuzi huo Prof. Gabagambi alikuwa Mhadhiri wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Kilimo – Sokoine (SUA).
Aidha Rais Magufuli amemteua Dkt. Deodatus Michael Mutasiwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, Dkt. Alphone Bilola Chandika kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma. Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Chandika alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Post a Comment