Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad amekutana na rais wa Rwanda, Paul Kagame siku ya Jumatatu ya Mach 12 huko Kigali ikiwa ni ziara yake ya siku tatu kwa nchi ya Afrika Mashariki.
Rais huyo wa CAF, Ahmad na mwenyeji wake, Paul Kagame wamezungumzia mambo mbalimbali yakiwemo maswala ya maendeleo ya kukuza soka la vijana katika bara la Afrika hasa kipindi hiki ambacho nchi ya Morocco ikiwa katika jitihada za kuandaa kombe la dunia mwaka 2026.
Rais Kagame ambaye amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa umoja wa Afrika katika mkutano wake wa 30 uliyohitimishwa huko Addis Ababa, nchini Ethiopia ameahidi kutumia nafasi hiyo kusaidia maendeleo na kukuza soka la Afrika.
Post a Comment