BABA AMZIKA MTOTO WAKE
Polisi wa Migori nchini Kenya wanachunguza kifo cha mtoto mwenye umri wa miezi
6, ambaye inasemekeana alifukiwa akiwa hai na baba yake mzazi.
Kwa mujibu wa kiongozi wa eneo hilo Chief Fredrick Owino, mwanaume huyo
aliyetambulika
kwa jina la Marcellus Odek, alirudi nyumbani kwake akiwa amelewa na kuchukua
jembe
na kuchimba kaburi, ambalo alimzika mtoto huyo ambaye ameelezwa alikuwa
akisumbuliwa
na tatizo la kupumua.
Taarifa zaidi zinasema kwamba mama wa mtoto huyo Annah Auma wakati tukio
linatokea alikuwa amepoteza fahamu kutokana na tatizo la kifafa alilokuwa nalo, na
alifanya tukio hilo mbele ya familia yake na majirani, usiku wa Machi 14 mwaka huu.
Ndugu wa familia hiyo Milicent Achieng amesema mtuhumiwa aliwakuta nyumbani
na moto akiwa anapumua, kabla hjaanza kuchimba kaburi na kumfukia, na alipoomba
msaada kwa watu walikataa nakumshauri akimbie kwani huenda angemuua na yeye.
Post a Comment