Header Ads

TSN yajivunia jukwaa la fursa za biashara








KAMPUNI ya magazeti ya Serikali (TSN) imesema, majukwaa ya biashara yanayofanyika kwenye mikoa mbalimbali nchini yanasaidia kuieleza dunia Tanzania ilivyo tayari kupata maendeleo na namna watu wa ndani na nje ya nchi wanavyoweza kushiriki ili nao wanufaike.




Kampuni hiyo inaendelea kuandaa jukwaa la fursa la biashara Zanzibar linalotarajiwa kufanyika Machi 15 mwaka huu kwenye ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi mjini Unguja.
Wawakilishi wa kampuni hiyo wakiwemo waandishi wa habari jana walikutana na kamati ya maandalizi ya jukwaa hilo inayoongozwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa Zanzibar, Bakari Ally Bakari. Jukwaa la Zanzibar ni la kwanza mwaka huu, na ni la tano tangu TSN ilipoanza kuyaandaa.
TSN pia imesema, majukwaa hayo yanaharakisha maendeleo ikiwa ni pamoja na kutangaza fursa za biashara na uwekezaji.
Mhariri Mtendaji wa magazeti hayo, Dk. Jim Yonazi amesema Kikwajuni mjini Zanzibar kuwa, TSN inajisikia fahari kupata fursa ya kutangaza fursa za biashara zilizopo visiwani humo.
Amesema, lengo la majukwaa ya biashara fursa za maendeleo na biashara zilizopo kwenye maeneo mbalimbali Tanzania, na kwamba, jukwaa la Zanzibar litasaidia kuelewa kisiwa hicho kinajiandaa vipi kwa ajili ya mabadiliko ya kiuchumi.
“Kwa hiyo sisi tunapeleka habari ambazo zinaweza zikasaidia katika kufanya maaumuzi” amesema Dk Yonazi na kubainisha kuwa, Zanzibar kuna fursa nyingi za utalii, za biashara na uwekezaji.
Kwa mujibu wa Dk Yonazi kufanyika kwa jukwaa la fursa za biashara Zanzibar kutaiwezesha dunia kufahamu kuna nini visiwani humo hasa wakati huu wa mabadiliko za kuiwezesha Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda.
“Tuna uhakika kabisa kwamba, kwa kufanya majukwaa haya ya biashara, au majukwaa ya kueleza fursa za biashara katika eneo la nchi yetu tunaiambia dunia jinsi ambavyo Tanzania ilivyo tayari kupata maendeleo lakini vilevile kuwapelekea Watanzania habari zao nje ili wenzetu wajue wanaweza kufanya nini Tanzania, fursa ziilizopo ni zipi” amesema Dk Yonazi.
Jukwaa la kwanza la biashara linaloandaliwa na TSN lilifanyika mkoani Simiyu Februari mwaka jana, likafuatiwa na la Mwanza, Tanga, na Shinyanga.
Zaidi ya watu 400 wamethibitisha kushiriki jukwaa la Zanzibar.
“TSN moja ya majukumu yake ni kupeleka habari za fursa za biashara, za serikali kwa wananchi na za wananchi kwa Serikali, lakini vilevile habari za biashara kwamba ni kitu gani kikifanyika tunaweza kupata maendeleo. Sasa TSN iliona kuwa kuna fursa kama hii ya kupeleka habari kwa watu ambazo zinaweza kuwasaidia kuleta maendeleo”amesema Dk Yonazi.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa TSN, kampuni hiyo, inapeleka kwa wananchi habari zenye zenye thamani na tija ziwawezeshe kufanya uamuzi.
Amesema, majukwaa ya fursa za biashara yanaandaliwa kitaalamu, yataendelea na amekaribisha washirikiane na TSN kuyaandaa kwa kuwa watanufaika na pia wataiwezesha nchi kupata maendeleo.
“Nchi hii ni yetu, maendeleo ni yetu, hakuna mtu atakayetusaidia maendeleo isipokuwa sisi, kwa hiyo tushirikiane” amesem

No comments