Roma Mkatoliki aomba kupunguziwa adhabu
BAADA ya kufungiwa kujihusisha na muziki kwa miezi sita na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) msanii wa muziki nchini, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ ameomba kupunguziwa adhabu hiyo kwani maisha yake yameanza kuwa magumu.
Roma alifungiwa kujihusisha na sanaa ya muziki baada ya kukaidi maagizo ya Basata yaliyomtaka kubadilisha maudhui aliyotumia kwenye wimbo wa ‘Kibamia’. Roma aliliambia gazeti hili juzi kwamba ataonana na katibu mkuu wa Basata ili kuangalia uwezekano wa kupunguziwa adhabu maana hali yake ya kiuchumi imeanza kuwa mbaya.
“Nataka niendelee kufanya muziki kwa sababu muziki unanisaidia kama ajira, nyuma yangu kuna watu ambao nawasaidia kwa hiyo wakati mwingine naomba ieleweke kwamba tufanye tu niendelee na muziki,” alisema Roma. Msanii huyo ambaye tayari ametumikia mwezi mmoja tangu kufungiwa alisema anajipa imani kupitia mkutano wa Baraza na Wasanii unaweza kufikiwa maamuzi ya kusamehewa.
Post a Comment