Header Ads

Türkische Armee rückt in Afrin ein
Rais Recep Tayyip Erdogan alisema bendera ya Uturuki na bendera ya wapiganaji wa upinzani wa Syria zimepandishwa katika mji huo, ambao hapo awali ulikuwa unadhibitiwa na kundi la wapiganaji wa Kikurdi linalojulikana kama Vikosi vya Ulinzi wa Raia, au YPG.

"Magaidi wengi walikuwa tayari wamekimbia," alisema Erdogan akiwa katika jimbo la magahribi mwa Uturuki la Cabakkale. Uturuki inavichukulia vikosi vya Kikurdi katika jimbo la Afrin lililoko mpakani mwake na Syria kuwa magaidi wenye mafungamano na kundi lililopigwa marufuku la 'Chama cha Wafanyakazi wa Kikurd' au PKK, ambalo limeendesha uasi ndani ya Uturuki kwa zaidi ya miongo mitatu.

Ankara ilianzisha operesheni dhidi ya mji wa Afrin na maeneo jirani Januari 20, na taratibu ilianza kuwasukumiza wapiganaji na mamia ya raia katikati mwa mji. Wanajeshi wasiopungua 46 wa Uturuki wameuawa katika operesheni hiyo.

Afisa wa Kikurdi, Hadia Yousef, aliliambia shirika la habari la Associated Press kuwa wapiganaji wa YPG hawajaukimbia mji huo, lakini waliwaondoa raia waliobakia "kutokana na mauaji." Alisema mapigano yalikuwa yanaendelea katika mji huo.

Shirika la uangalizi wa haki za binadamu la Syria lenye makao yake nchini Uingereza lilisema vikosi vinavyoungwa mkono na Uturuki vimechukuwa udhibiti wa nusu ya mji huo, huku mapambano makali yakiendelea.


Safishasafisha ya mabomuShirika hilo linasema karibu watu 200,000 wameikimbia Afrin katika siku za karibuni kuepuka mashambulizi makali ya ndege, na kuingia eneo jirani lililoko chini ya udhabiti wa serikali ya Syria. Televisheni ya Syria ilionyesha picha siku ya Jumapili, za msafara mrefu wa magari na raia watembeayo kwa miguu wakiondoka Afrin. Erdogan amesema wakaazi wa Afrin watarejea.

Jeshi la Uturuki wakati huo liliarifu kupitia mtandao wa twitter kuwa lilikuwa linaendesha operesheni za kutafuta mabomu ya ardhini pamoja na miripuko. jeshi liliweka video kwenye mtandao wa kijamii ikimuonesha mwanajeshi aliebeba bendera ya Uturuki na mwanaume anaepeperusha bendera ya upinzani wa Syria kwenye roshani jengo la bunge la wilaya, huku kukiwa na kifaru kilichoegeshwa mtaani.

Mwanajeshi huyo aliitaja hatua ya kutekwa kwa jimbo la Afrin kuwa zawadi kwa taifa la Uturuki na kwa wanajeshi waliouawa katika kumbukumbu ya ushindi maarufu wa vita kuu vya kwanza vya dunia. Picha za shirika binafsi la habari la Uturuki la Dogan, zilionesha wapiganaji wa Syria wakifyatua risasi hewani kusherehekea ushindi
.
Tovuti za habari za Kikurdi zilionesha picha za wapiganaji wakiharibu sanamu inayoashiria sherehe za mwaka mpya wa Kikurdi zinazofanyika wiki hii. Sanamu hiyo ni ya Kawa, ambaye ni shujaa wa kubuniwa katika milima ya Zagros nchini Iran aliemshinda mtawala katili na kuwasha mioto kueneza habari, za kuanza kwa majira ya machipuko.


Türkische Armee rückt in Afrin ein
chanzo dw swahili

No comments