kikosi kipya Taifa Stars
Baada ya hivi karibuni kocha wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania Salum Mayanga, kutaja kikosi cha wachezaji watakaocheza mechi mbili za kimataifa za kalenda za FIFA kwa mwezi Machi, mshambulijai Thomas Ulimwengu ameondolewa.
Awali mshambuliaji huyo wa klabu ya soka ya AFC Eskilstuna ya nchini Sweden alikuwa amejumuishwa kwenye kikosi hicho kitakachocheza dhidi ya Algeria na baadae DR Congo lakini taarifa ya kikosi iliyotolewa na TFF leo jina lake halipo.
Kikosi hicho sasa kina wachezaji 21 wakiwemo nyota watatu wa kimataifa wa Tanzania, nahodha Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubeligji, Simon Msuva anayecheza Diffa El Jaddida ya Morocco pamoja na Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini.
Taifa Stars itasafiri hadi Algeria kucheza mechi hiyo ya kirafiki Machi 22 kabla ya kurejea Tanzania kucheza na DR Congo Machi 27 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Sababu za kuondolewa kwenye kikosi hicho kwa Ulimwengu ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu baada ya kuwa majeruhi hazijawekwa wazi.
Post a Comment