Header Ads

WANANCHI zaidi ya 2,000 wanaoshi kwenye vijiji vitatu vilivyopo Kata ya Sinya, Tarafa ya Enduimet Wilayani Longido wamezingirwa na maji


Image result for Longido


WANANCHI zaidi ya 2,000 wanaoshi kwenye vijiji vitatu vilivyopo Kata ya Sinya, Tarafa ya Enduimet Wilayani Longido wamezingirwa na maji kwa muda wa siku 15 sasa na kukosa huduma muhimu za afya, shule na mahitaji mengine.
Mbunge wa Jimbo la Longido, Dk Stephen Kiruswa na mfanyabiashara wa bidhaa mbalimbali, Philemon Mollel wametoa msaada wa unga mifuko 255 kwa ajili ya kusaidia wananchi hao kupata chakula.
Akikabidhi msaada huo jana katika kijiji cha Leremeta ambacho ni mojawapo kati ya vijiji vilivyozingirwa na maji, Dk Kiruswa alisema wananchi hao wamezingira na maji na hawawezi kufanya shughuli yoyote.
Alisema mafuriko hayo yametokea kwenye Milima ya Engarinaibor, Longido, Namanga na Kilimanjaro kisha kujaa kwenye kijiji hicho na kusababisha kaya 255 zenye watu zaidi ya 2,000 kushindwa kupata huduma muhimu.
Dk Kiruswa amesema, ameamua kutoa msaada huo wa unga wa chakula kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hao na kwamba atapeleka msaada wa boti mbili zitakazowasaidia kusafirishwa kwenda hospitali, sokoni au kwenda kufanya shughuli nyingine muhimu.
Naishoro Olorina mmoja kati ya wananchi walioathirika, ameshukuru na kusema, hawakuwa na chakula wala mahitaji mengine na wanashindwa kwenda kununua mahitaji yao kwa sababu ya maji hayo.
Awali Ofisa Tarafa wa Kata ya Enduimet, Lekishon Lengoye alishukuru kwa msaada huo na kuomba wadau wengine kujitokeza kisaidia wananchi hao.

No comments