Header Ads

Jeshi la polisi linamshikiria Selemani Masoud(68) mkazi wa Yombo Kilakala kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka mbalimbali za serikali











Jeshi la polisi linamshikiria Selemani Masoud(68) mkazi wa Yombo Kilakala kwa tuhuma za kukutwa na nyaraka mbalimbali za serikali ikiwemo kughushi mihuri na vyeti feki na vyuo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda Mambosasa amesema kuwa Marchi 13, mwaka huu Jeshi hilo taarifa ya Kiitelijensia kuwa kuna kundi la watu linalojihusisha na kutengeneza vyeti feki, mihuri na nyaraka mbalimbali za serikali katika eneo hilo.
Makachero wa kikosi kazi cha polisi walifika eneo la nyumba ya mtuhumiwa na kuanza upekuzi katika nyumba ya mtuhumiwa huku wakishirikiana na uongozi wa serikali za mtaa kufanikisha kumkamata mtuhumiwa na nyaraka hizo.
Mtuhumiwa alikutwa na nyaraka mbalimbali ambazo ni Mihuri 53, ukiwemo wa Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA), Mhuri wa VETA, Chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM, Chuo cha Sokoine (SUA),Chuo cha Bandari, Chuo Kikuu cha Huria cha Tanzania(OUT), Mtwara University, Muhuri wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA),Muhuri wa cancelor wa UDSM, Chuo cha Usafirishaji (NIT),Chuo cha usimamizi wa Fedha (IFM), Bodi ya uhasibu(NBAA), Chuo cha Tumaini(TUDARCO), Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, RITA, Health Laboratory, JKT Makao makuu, Marine Association of certified.
Mwingine wa Mahakama ya Kisutu, Chuo cha uhasibu Arusha, Chuo cha utumishi wa umma,muhuri ya maliasili na utalii, Mkurugenzi wa Jiji Eastern London, Mkuu wa shule Marangu, Mkuu wa shule ya songambele, Mbagala Nursing, Msajili wa Ndoa, Shule ya Magereza, Medical Board of Tanganyika, Mkuu wa shule Kaselya Sec, Glory of Nursing, Director of Tanzania public service,Shule ya Sekondari Kibasila, Afisa Elimu mkoa wa Kilimanjaro, Mwalimu mkuu shule ya Msingi Mgulani, Mkuu wa shule Kyaka sekondari.
Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi ili kubaini mtandao mzima anaoshirikiana nao ili kuhakikisha linawatia mbaroni wote hata kama ni watumishi wa umma.

No comments