Header Ads

Chama tawala cha National People's Congress nchini China, leo Jumapili, kinatarajia kuidhinisha marekebisho

Xi Jinping claps, looking slightly to the side of the frame
Chama tawala cha National People's Congress nchini China, leo Jumapili, kinatarajia kuidhinisha marekebisho ya kipengee cha katiba, ya kufutilia mbali uongozi wa mihula miwili kwa Rais wa nchi hiyo.
Hatua hiyo sasa itamfanya Rais Xi Jinping, kusalia mamlakani hata baada ya muhula wake wa pili kumalizika mnamo mwaka 2023 na kuendelea kuongoza kwa kipindi kisichojulikana.
Wakosoaji wameonya kuhusiana na hatari ya kuondoa muda wa mihula miwili ya uongozi wa Rais, ambayo ililetwa na Deng Xiaoping mwaka 1982.
Chama hicho kinasema kuwa, mabadiliko hayo yataupa nguvu na kuboresha mfumo wa uongozi nchini humo.
Yeyote anayepinga mabadiliko hayo, kwa hofu kuwa itampa nguvu zaidi mtu mmoja, amezimwa nchini humo.

No comments