Header Ads

MMILIKI WA MABASI YA SUPER SAMI AKUTWA AMEKUFA MTONI

 MMILIKI WA MABASI YA SUPER SAMI AKUTWA AMEKUFA MTONI



Mwili wa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah unaodaiwa kukutwa mtoni ukiwa umefungwa kwenye mfuko wa sandarusi
Mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah enzi za uhai wake


Image result for abasi ya Super Sami, Samson Josiah









Habari tulizozipata hivi punde zinasema mwili wa Mmiliki wa mabasi ya Super Sami Samson Josiah umekutwa katika mto Ndabaka eneo la Bunda /Lamadi.

Taarifa kutoka vyanzo vya habari vya Malunde1 blog ni kwamba mwili wa Samson Josiah umeokotwa na wavuvi wa samaki leo jioni Jumatano Machi 14,2018.

Watu wa karibu na marehemu wanasema mwili uliookotwa ni wa Samson Josiah.

Taarifa zaidi tutawaletea hivi punde...

Miongoni mwa habari zilizoteka vyombo vya habari Tanzania tangu Machi 9, 2018 hadi ni kuhusu kupotea kwa mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah kwa zaidi ya wiki mbili sasa.

Mapema ilielezwa kuwa gari yake ndogo aliyokuwa akiitumia aina ya Toyota LandCruiser ilikutwa imechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyoko mkoani Mara siku ya Machi 9, lakini yeye mwenyewe alikuwa hajapatikana.

Kwa mujibu wa familia ya Bwana Josiah, ambayo inaishi mkoani Mwanza, ilidai kuwa siku ya kupotea kwa Josiah ambayo ni February 27, majira ya usiku, Josiah alimpigia simu mkewe na kumwambia kuwa atarudi nyumbani na mgeni, na hayo yakawa mawasiliano yao ya mwisho.

Mabasi ya Super Sami yanafanya safari zake kuanzia mkoa wa Mwanza, kwenda mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa pamoja na Kagera.

No comments