hadija Omary Abdallah Kopa hatoa ya moyoni
Hayo ameyasema Bi. Khadija mapema leo alipokuwa katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia kurasa za EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri.
Khadija amesema kuwa ndani ya CCM nafasi kubwa aliyowahi kuishika ni kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu CCM kwa muda wa miaka 10 na kwa sasa hatamani kugombea nafasi nyingine kwa kuwa ndoto zake za kuwania ubunge zilishakatika tangu aliposhindwa kuingia bungeni miaka iliyopita.
Mkongwe huyo amefafanua kwamba hakufikiria kama angekosa nafasi ya kwenda bungeni kwani kipindi hicho alikuwa akijitahidi kuwa mbele sana katika kufanya kazi za chama lakini uchaguzi ulipofika wenzake walimpita kwa kuwa walikuwa wana tumia vitu vya thamani kushawishi huku yeye akiwa hana.
Aidha Bi. Khadija ameongeza kwamba pamoja na kuwa kwa sasa hana nafasi ya Uongozi CCM hawezi kukihama chama hicho kwani hapo ndipo alipofika na haoni mahali pengine kwa kwenda.
Post a Comment