Header Ads

Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa amekiri kufurahishwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu


Image result for Edward Lowassa


Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA, Edward Lowassa amekiri kufurahishwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa kwamba kauli yake aliyoitoa juzi akitaka kuwepo kwa mjadala wa kitaifa kujadili hali ya elimu nchini.

Lowassa ametoa kauli hiyo leo Machi 19, 2018 katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa na msemaji wake, Aboubakar Liongo ambapo amesema kwamba ajenda ya kuwepo mjadala wa kitaifa ilikuwa ajenda yake tangu alipokuwa CCM na hata alipoingia CHADEMA alizidi kuliendeleza.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba Lowassa amesema amesoma na kusikia taarifa ya Mkapa akitaka kuwepo kwa mdahalo wa kitaifa kuhusu kushuka kwa elimu nchini lakini amedai kuwa ajenda hiyo sio ya CCM na hawataweza kuisimamia kwa sababu wanataka kuendelea kutawala,ila hawataki Taifa lililoelimika vizuri na linaloweza kuhoji.

“Nimefurahi kuwa Mkapa ameliibua suala hili kwani hiyo ilikuwa ni ajenda yangu ya kwanza tangu nikiwa ndani ya CCM na nje ya CCM. Pia Ilani ya uchaguzi ya CHADEMA, elimu ndio ilikuwa ajenda kuu na tulisema tutaita mjadala wa kitaifa kuhusu elimu na kuangalia wapi tumekwama na nini kifanyike,” amesema Lowassa.

No comments