Header Ads

Azam fc yatangaza vita

Baada ya timu ya Azam FC kuichapa bao 1-0 Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu usiku kuamkia leo, klabu hiyo imetangaza vita kwenye michezo yake ijayo kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Image result for Uwanja wa Azam Complex.






''Tunamshukuru Mungu kwa kuzoa pointi tatu dhidi ya Singida United. Hivi sasa akili yetu yote tunaiweka kwenye mechi mbili zijazo dhidi ya Mwadui alhamisi ijayo na Mbao Jumapili ijayo, zote zikifanyika Azam Complex saa 1.00 usiku'' imeeleza taarifa ya Azam FC.
Bao pekee la ushindi katika mchezo wa jana lilifungwa na  Joseph Mahundi baada ya kazi nzuri iliyofanywa na mshambuliaji aliyesajiliwa msimu huu akitokea Kagera Sugar Mbaraka Yussuf dakika ya 17.

Image result for Uwanja wa Azam Complex.


Baada ya ushindi wa jana Azam SASA imefikisha pointi 38 baada ya kucheza mechi ya 20,  ikizidiwa pointi mbili tu mabingwa watetezi, Yanga walio nafasi ya pili kwa pointi zao 40 za mechi 19, nyuma ya SImba wanaoongoza kwa pointi 46 kwenye mechi 20.

Image result for Uwanja wa Azam Complex.

No comments