Header Ads

CHINA, taifa lenye jumla ya watu takribani bilioni 1.4,


Image result for CHINA,


CHINA, taifa lenye jumla ya watu takribani bilioni 1.4, inayopatikana Asia ya Mashariki, inabaki kuwa nchi pekee duniani yenye siasa za kipekee kabisa. Hiki ni kipindi muhimu sana katika siasa za nchi hii ambayo kwa mujibu wa rekodi za Benki ya Dunia, ni taifa la pili duniani kwa kuwa na uchumi mkubwa.
Mkutano wa Bunge la Umma la China limeketi rasmi kuanzia leo (Jumatatu), pamoja na mambo mengine, kukamilisha shughuli zake za kikatiba. Akizungumza na maelfu ya waandishi wa habari kutoka takribani kila pembe ya dunia jana, msemaji wa mkutano huu wa Bunge la Umma la China Zhang Yesui, alibainisha kuwa chombo hicho cha juu kabisa chenye mamlaka ya mwisho juu ya serikali na utendaji wake unakaa kukamilisha majukumu yake ya msingi.
Mwaka huu, pamoja na kazi nyingine, mkutano huo utashughulikia marekebisho ya katiba, kufatilia mchakato wa maendeleo kwa ujumla na kutoa mapendekezo kuhusu utekelaji wa mpango wa maendeleo ya China. Macho yote ya dunia kwa sasa yameelekezwa katika matukio makubwa ya kisiasa yanayoendelea hapa jijini Beijing, sababu kubwa ikiwa ni kuwa taifa hili ni miongoni mwa mataifa makubwa yanayogusa moja kwa moja mustakabali wa ustawi wa nchi zinazoendelea hasa za bara la Afrika.
Baada ya mkutano wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa, kukaa siku ya Jumamosi, Bunge la Umma la China linakaa sasa ikiwa ni chombo kikuu kabisa cha kikatiba cha kufanya maamuzi yote yanayohusu taifa. Hiki ndicho chombo kinachochagua rais, serikali, kamati kuu ya kijeshi na mwanasheria mkuu. Vilevile, kama ilivyokuwa na uwezo wa kuwateua hao ndivyo ambavyo pia kimepewa madaraka ya kuwafukuza kazi mara moja pale inapothibitika kwenda kinyume na maslahi na matakwa ya taifa.
Nini kinafanya siasa za China kuwa za kipekee? Ni swali la kawaida lakini zito; kwanza pamoja na kuwa taifa hili linaongozwa na chama cha Kikomunisti, lakini pia kuna vyama vingine vya kidemokrasia vinane. Hivi vyama vyote ni sehemu ya maamuzi na vinaunga mkono chama tawala cha Kikomunisti.
Kwa siasa za Afrika, ni vigumu kukuta chama kisichokuwa madarakani kuunga mkono juhudi za chama tawala, isipokuwa pale tu panapotokea kutoelewana na kulazimika kuunda serikali ya umoja wa kitaifa. Lakini upekee mwingine katika siasa hizi ni namna bunge lilivyopewa madaraka makubwa sana. Kwa nchi hii, bunge ni mamlaka na mamlaka ni bunge! Kama hili halitoshi, kutofautisha bunge na chama siyo kazi rahisi. Bunge la umma la China, kiuhalisia, maazimio yake yote ni utekelezaji tu wa maazimio ya uongozi wa chama cha kikomunisti ambacho ndicho chama tawala.

No comments