Header Ads

WATU wenye matatizo ya fizi wapo hatarini ya kupata magonjwa ya kisukari


Image result for WATU wenye matatizo ya fizi

WATU wenye matatizo ya fizi wapo hatarini ya kupata magonjwa ya kisukari na moyo, utafiti wabainisha.
Kutokana na changamoto hiyo, madaktari wa kinywa na meno nchini wameandaa programu ya kuchunguza afya ya kinywa na meno kwa baadhi ya mikoa hapa nchini Hayo yamebainishwa na Rais wa Chama cha Madaktari wa Meno nchini, Dk Ambeje Mwakatobe wakati akizungumza na wanahabari hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam.
Mwakatobe amesema kuwa katika kuadhimisha siku ya afya ya kinywa na meno ambayo hufanyika Machi 20 kila mwaka chama hicho ambapo, mwaka huu kimepanga kufanya uchunguzi na kutoa elimu ya afya ya kinywa na meno katika mikoa 22 ya Tanzania bara na Visiwani.
Aidha Dkt Mwakatobe amesema kuwa wamepanga kutoa uchunguzi pamoja na elimu ya afya ya kinywa na meno kwa zaidi ya watu 70,000 huku walengwa wakuu wakiwa ni watoto, watu wenye mahitaji maalum na wale wanaoishi katika mazingira magumu Maadhimisho ya siku ya afya ya kinywa na meno yatafanyika mkoani Mara huku kaulimbiu ya mwaka huu ikiwa “Sema ah Fikiri Kinywa, Fikiri Afya.”

No comments