Header Ads

faru pekee wa kiume aina ya Northern White Rhino aliyekuwa amesalia hai duniani, amekufa akiwa na umri wamiaka miaka 45


Huyu ni faru pekee wa kiume aina ya 'Northern Whire Rhino' aliyesalia ulimwenguni
faru pekee wa kiume aina ya Northern White Rhino aliyekuwa amesalia hai duniani, amekufa akiwa na umri wamiaka  miaka 45
Faru huyo alikuwa akitibiwa kwa muda na matabibu katika shamba kubwa la uhifadhi wa wanyama la kituo hicho kwa muda kutokana na matatizo yaliyotokana na kuzeeka kwake.
Alikuwa na vidonda ambavyo vilikuwa vinakosa kupona kutokana na umri wake.
Shirika la Ol Pejeta limesema hali yake ilidhoofika sana katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
"Hakuweza hata kusimama na alikuwa anateseka sana," Ol Pejeta wamesema kupitia taarifa.
Matabibu wa wanyama kutoka kituo cha uhifadhi wa wanyama cha Dvur Kralove kutoka Jamhuri ya Czech, Ol Pejeta na Shirika la Wanyamapori kenya waliamua kukatisha uhai wake."
Sudan alikuwa maarufu sana duniani na alikuwa nembo ya kutetea juhudi za kupigana na ujangili na kuwaokoa wanyama walio katika hatari ya kuangamia.

No comments