Wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto imethibitisha kulipuka tena kwa ugonjwa wa Dengue
Wizara ya Afya, Jinsia, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto imethibitisha kulipuka tena kwa ugonjwa wa Dengue ambao uliwahi kuibuka nchini na kuua baadhi ya watu.
Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv , msemaji wa Wizara ya Afya Nsachris Mwamwaja, amesema ni kweli ugonjwa huo umeripotiwa kuibuka tena, na taarifa kamili inatarajiwa kutolewa leo mchana na Waziri Ummy Mwalimu.
“Na kweli Katibu Mkuu aliitoa, lakini rasmi tutaoa wakati wowote leo, kuna shughuli ambayo ataifanya Waziri kwa hiyo kuna uwezekano akatoa taarifa hiyo kwa sababu imeshandaliwa”, amesema Bwana Mwamwaja.
Ugonjwa huo ambao unasababishwa nakirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes., husababisha homa kali na hatimaye kifo, hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na kutumia vyandarua wakati wa kulala, na kuepuka kukaa sehemu zenye mbu.
Chanzo- EATV
Post a Comment