Header Ads

aganga wa kienyeji katika kuwagundua wagonjwa hao (TB)




Katika kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) nchini, serikali imesema kuwa itawa
tumia waganga wa kienyeji katika kuwagundua wagonjwa hao ili waweze kufikishwa kwenye vituo vya afya na kupata tiba sahihi.

Kauli hiyo imetolewa leo (Mchi 23, 2018) mjini Dodoma na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani yatakayofanyika kesho (Machi 24, 2018).
Waziri Mwalimu amesema kuwa waganga wa kienyeji ni wadau muhimu katika kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu kwa kuwa wagonjwa wengi hukimbilia kwao kwa kudhani kuwa wamerogwa.
Aidha, Ummy amesema kwa mujibu wa takwimu za shirika la afya duniani WHO inakadiriwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua kifua kikuu kila mwaka duniani huku milioni moja kati yao wakiwa ni watoto wenye umri chini ya miaka 15 na hapa nchini kila mwaka jumla ya watu 60,000 wanaambukizwa ugonjwa huo wakati mwaka 2016 watu 65,908 waliogundulika kuugua na kuanza matibabu.

No comments