Takukuru mkoani tabora imeokoa milioni miamoja lakisaba elfusitini na themani na sita
Takukuru
mkoani tabora imeokoa milioni miamoja lakisaba elfusitini na themani
na sita kutoka kwa wadau mbalimbali
Akizungumza
na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa takukuru mkurungezi wa takukuru mkao watabora MOGASA
MOGASA amesemakuwa wamefanikiwa kuokoa fedha hizo katika kipindi cha julai 2017
mpaka februali 2018.
MOGASA
ameasema kuwa licha ya kuwepo kesi mahakamani lakini kuna kesi zingine
wanashindwa na zingine wanashinda kutokana mashahidi kuosekana mahakamani
inapelekea takukuru kushindwa kesi
AIDHA
mkurungezi wa takukuru MOGASA MOGASA
amewataka wananchi kushirikiana na takukuru kwa uaminifu na wala
wasiogope kutoa tarifa wanapoona sehem frani kuna rushwa inatokea kwani takuru
ipo kwajili ya watu wote
Uwepo wa
taarifa za maandishi au za mdomo kuhusu kugawanya mirathi pale mwenye mali
anapofariki dunia huondoa migogoro katika familia na jamii kwa jumla.
Akizungumza
Wakili wa Kujitegemea katika Ofisi ya Wakili MTAKI,Wakili TERESIA FABIAN
amesema wosia unapoachwa na marehemu unapunguza migogoro inayoweza kujitokeza
katika familia.
Naye
Mwanamke aliyedhulumiwa mali na ndugu wa marehemu mume wake katika kijiji cha
IGALULA wilayani UYUI,MWAJUMA ALI amesema baada ya mume wake kufariki dunia
bila kuacha wosia ndugu wa marehemu walichukua mali zote na kumwacha na watoto
wanne bila msaada wowote.
Kwa upande
wake,Mwanasheria kutoka Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu,YUSUPH
SALMIN anaeleza ni kwa jinsi gani wanawasaidia wahanga wanaodhulumiwa mirathi.
Afisa
Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Manispaa ya TABORA,ENEMBORA LEMA amesema
wao kama serikali wanatoa elimu na kuwaelekeza namna ya kupata msaada wa
kisheria wahanga wa mirathi.
Ameongeza
kuwa wananchi wanapoandika mirathi wanapata uhakika wa kuacha mali au vitu vyao
katika sehemu salama.
………….
KIMATAIFA
Maafisa wa
Mamlaka ya Taifa ya Usalama Barabarani (NTSA) pamoja na Shirika la Msalaba
Mwekundu Kenya wametoa ushauri ambao unaweza kukufaa sana wakati huu wa mvua.
1. Fahamu kwamba wakati wa kiangazi,
vumbi, mchanga na taka za aina mbalimbali hurundikana barabarani. Mvua
inaponyesha, husababisha barabara kuwa telezi na kwa hivyo ukiwa na gari ni
muhimu kutoendesha gari lako kwa mwendo wa kasi kupindukia kwani gari
likiteleza utashindwa kulidhibiti gari lako kwa urahisi.
2. Kwa sababu ya maji, huwa vigumu sana
kupiga breki wakati wa mvua na hivyo hatari ya mwenye gari kumgonga anayetembea
barabarani huwa juu. Unashauriwa kutoendesha gari kwa mwendo wa kasi.
3. Kwa sababu ya mvua, wapita njia mara
nyingi hutembea wakiwa wameinamisha vichwa chini na huenda wasilione gari
linapokaribia. Wenye magari wanashauriwa kuwa makini zaidi wanapofika kwenye
vivuko barabarani au wanapomuona mtu akivuka barabara. Kwa wanaotembea kwa
miguu, wanashauriwa kutumia vivuko vilivyotengwa na kuchukua tahadhari zaidi
pia.
4. Kwa wenye magari, iwapo barabara
imefurika maji, ni vyema kutafuta barabara nyingine ya kupitia badala ya
kujaribu kupitia ndani ya maji. Huwa vigumu kukadiria kina cha maji barabara
inapofurika.
5. Wakati mvua inaponyesha, wenye magari
wanatakiwa kuwasha taa kuwawezesha kuona mbele na pia kutokaribia sana magari
yaliyo mbele yao. Maji yanayorushwa na gari lililo mbele yanaweza kutatiza
mwenye gari iwapo atakuwa karibu sana. Ushauriwa kufuata kanuni ya sekunde 3,
hicho ndicho kipindi kinachochukuliwa na binadamu kuona jambo na kuchukua
hatua. Usipofanya hivi, kufikia wakati unapoona aliye mbele yako amesimama na
kuchukua hatua utakuwa tayari umesababisha ajali.
6. Breki za gari huathiriwa na maji, kwa
hivyo unapoendesha gari eneo lenye maji, ni vyema kuendesha gari kwa mwendo wa
polepole. Hii itaziwezesha breki kukauka.
7. Madereva wanashauriwa pia kutumia
mikono yao miwili kudhibiti mwelekeo wa gari kuhakikisha wanadhibiti vyema
gari.
8. Wapita njia, waendesha baiskeli na
waendeshaji pikipiki wanashauriwa kuvalia mavazi yanayoweza kuonekana vyema au
mavazi yanayoweza kuakisi mwanga. Haya yatamuwezesha mtu kuonekana na madereva
na kumpungushia mtu hatari ya kugongwa.
9. Usiendeshe gari lako ndani ya maji
yanayosonga, yawe kwenye mifereji au kwenye mto. Huwa vigumu sana kukadiria
nguvu ya maji. Magari mengi husombwa na maji madereva wakijaribu kuvuka mito au
wakitumia madaraja yaliyofurika maji. Mvua pia hudhoofisha madaraja, jambo
ambalo huenda usifahamu. Daraja linaweza kubomolewa bila ufahamu wake wewe nawe
ukaingia mtoni ukitarajia daraja bado lipo. Maji ya kina ya futi moja yanaweza
kusomba gari lako. Kwa binadamu anayetembea, inchi sita za maji zinaweza
kukusomba.
10.
Ukiwa
na gari lako, hakikisha vipangusia kioo vya gari lako vinafanya kazi. Hili litakuwezesha kupangusa
kioo na kuona mbele unapokuwa barabarani.
11.
Iwapo
una gari na limeanza kuteleza, achilia mafuta na kulielekeza gari upande ambao
unateleza. Ukianfanikiwa kudhibiti gari, anza kulainisha magurudumu tena na
kurejea barabarani. Hakikisha kwamba unabaki kuwa tulivu na usichukue hatua
yoyote ghafla.
12.
Usiende
kwa mwendo wa kasi. Iwapo una safari ya mbali, anza mapema kuhakikisha kwamba
haukumbwi na shinikizo la kutaka kwenda kwa kasi ndipo ufike.
13.
Unapokuwa
unaendesha gari, usishawishike kutumia simu yako au kufanya jambo lolote ambalo
litakuzuia kuwa makini ukiliendesha gari.
14.
Iwapo
utakuwa safarini, usiegeshe gari lako au kuanza kufanya shughuli zako karibu na
mto wakati wa mvua.
15.
Ni
vyema kusikiliza vituo vya redio na runinga kujifahamisha kuhusu yanayojiri na
ni wapi mvua kubwaimenyesha au mafuriko kutokea.
16.
Usitembee
kwenye maji au maeneo yenye matope ambayo kuna uwezekano kwamba kuna nyaya za
umeme ambazo zimeanguka. Nyumba yako ikifurika maji pia, hakikisha umezima
stima.
17.
Iwapo
unatembea kwa miguu, tumia fimbo au kijiti kukadiria kina cha maji.
18.
Mafuriko
yakitokea eneo ulipo, mara moja kimbilia maeneo yaliyo juu na salama.
Post a Comment