Ukatili wa kingono kwa wanaume umepungua
Ukatili wa kingono kwa wanaume umepungua kutokana wanawake kuwatunza waumme zao kwa kuwapa haki yao ya msingi ya ndoa, huku takwimu zikionesha toka mwaka 2009 mpaka mwaka huu kuna kesi tatu za wanaume kunyimwa tendo la ndoa tofauti na hapo awali.
Akizungumza mapema hii leo Mratibu wa Ushauri na Msaada Kisheria katika Shirika la JABOYA lililopo Ilemela jijini Mwanza Bw. Emmanuel Mhoja, alisema hapo awali walikuwa wanapokea kesi nyingi za ukatili wa kingono, kwa sasa imepungua kutokana na elimu imewafikia ipasavyo jamii imebadilika kwa kiasi kikubwa.
"ukatili wa kingono umepungua kutokana na jamii kupata elimu ya kutosha, japo wanawake wanaongoza kwa kesi nyingi, tofauti na wanaume ambapo akinyimwa haki yake ya ndoa anatafuta nyumba ndogo jambo linalochangia maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi," alisema Mhoja.
Mhoja alisema, kesi ya mwisho kufikishwa ofisini hapo kunyimwa tendo la ndoa kwa mwanaume ni kutokana na maisha duni ambapo mwanamke alikuwa anamnyima tendo la ndoa mme wake, kwa sababu walikuwa wanalala chumba kimoja na watoto wao wenye umri mkubwa.
Aidha, ametoa rai kwa jamii kuachana na michepuko kwani eneo la Kanda ya Ziwa Victoria takwimu zinaonesha maambukizi ya virusi vya Ukimwi iko juu zaidi, jambo linalopelekea watoto kuishi ktika mazingira magumu.
IMEANDIKWA NA MWANDISHI WETU
James Timber
Post a Comment