Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup
Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) inatarajiwa kuchezwa mwishoni mwa mwezi Machi katika viwanja vinne tofauti nchini.
Ijumaa Machi 30, 2018 kutakuwa na mchezo mmoja katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, ambapo wenyeji Stand United watawakaribisha Njombe Mji majira ya saa 10:00 jioni.
Machi 31, 2018 kutakuwa na michezo miwili, Tanzania Prisons watakuwa wenyeji wa JKT Tanzania saa 8:00 mchana uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, huku saa 2:00 usiku Azam FC watakua wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam.
Jumapili Aprili Mosi, 2018 kutakuwa na mchezo mmoja, Singida United watakuwa wenyeji wa Young Africans katika uwanja wa Namfua mjini Singida Aprili Mosi, 2018 mchezo utakaonza saa 10:00 jioni.
Post a Comment