Header Ads

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema, jukwaa la fursa za biashara Zanzibar




Image result for Dk. Harrison Mwakyembe


WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema, jukwaa la fursa za biashara Zanzibar ni tukio muhimu kwa nchi na ni la aina yake kufanyika visiwani humo.
Dk. Mwakyembe ameyasema hayo leo mjini Unguja alipozungumza wakati wa ufunguzi wa jukwaa hilo la kwanza la fursa za biashara tangu Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ilipoanza kuyaandaa Februari mwaka jana mkoani Simiyu.
Amempongeza Mhariri Mtendaji wa TSN, Dk. Jim Yonazi kwa ubunifu na uthubutu wa kuandaa majukwaa kama hayo.
Kwa mujibu wa Waziri Mwakyembe, majukwaa hayo yanaibua mawazo chanya na kuwezesha washiriki kuzibaini fursa za maendeleo.
Dk. Mwakyembe amesema, mwitikio wa majukwaa ya fursa za biashara umekuwa mkubwa na mahitaji bado ni makubwa.
Amesema, Zanzibar bado haijatumia fursa za maendeleo zinazoweza kubadili hali ya uchumi wa wananchi na nchi kwa ujumla.
Hata hivyo amempongeza Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein kwa kuwa uchumi wa visiwa hivyo umekuwa ukikua mwaka hadi mwaka.
Waziri Mwakyembe amesema, wizara anayoiongoza unaunga mkono juhudi za TSN kwa sababu ya nguvu kubwa ya elimu katika majukwaa hayo inayoweza kuhamasisha wananchi wazitumie fursa.
Ametoa mwito kwa asasi na taasisi zenye mwelekeo wa kibiashara zishirikiane na TSN ili fursa ya majukwaa iwafikie wananchi wote.

No comments