Header Ads

KiIJANA aliyetajwa kwa jina la Festa Mtunga anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 36

Image result for JENEZa

KiIJANA aliyetajwa kwa jina la Festa Mtunga anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 30 hadi 36 amekutwa amekufa kwenye nyumba ya kulala wageni Chalinze mkoani Pwani.
Hadi sasa haijafahamika kijana huyo ni mkazi wa wapi.
Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Jonathan Shana, amewaeleza waandishi wa habari ofisini kwake mjini Kibaha kuwa, tukio hilo lilitokea Machi 27 mwaka huu, saa 4:00 asubuhi huko Chalinze.
Shana amesema Festa alilala kwenye nyumba hiyo lakini ilipofika asubuhi wahudumu walimgongea mlango bila ya mafanikio na ndipo walipotoa taarifa polisi.
"Polisi ilibidi wavunje mlango na kumkuta akiwa amelala peke yake kitandani, hakuwa na jeraha lolote mwilini mwake baada ya uchunguzi na kuondoa mashaka juu ya kifo chake," amesema.
Ametoa mwito kwa ndugu wa marehemu kujitokeza kuuchukua mwili huo.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Tumbi.

No comments