Header Ads

watu watano wapoteza maisha



WATU watano, wakiwemo wanawake wanne na mwanamume mmoja ambaye ni dereva wa basi dogo aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T 962 BSE 

aliyetambuliwakwa jina la Jackson Adam, wamekufa papo hapo baada ya basi hilo kugongana na basi la New Force.
Basi hilo lenye namba za usajili T 346 DLY, lilikuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Tunduma. Ajali hiyo pia ilisababisha majeruhi tisa ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu.

Miongoni mwa wanawake waliopoteza maisha ni pamoja na Witness Mwamuni (26) ambaye watoto wake wawili aliokuwa akisafiri nao kwenye basi hilo dogo wamejeruhiwa na kulazwa Wodi Namba Nne katika hospitali hiyo.

No comments