Header Ads

Kikwete awakumbuka wananchi wake


Related image

Mbunge wa Chalinze (CCM) Mhe. Ridhiwani Kikwete amefunguka na kumshukuru Rais 
mstaafu wa awamu ya nne Mzee Jakaya Kikwete na mkewe wake kwa kuweza 
kuchangia mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati na Nyumba za walimu.

Ridhiwani ametoa salamu hizo za pongezi kwa Mzee Kikwete na Mama Salma wakati alipokuwa anazungumza katika mkutano wake na wananchi wa Jimbo la Chalinze eneo la Kibindu.
"Maaara Paap. Mbunge wa Zamani/Mkulima kaibuka Mkutanoni.Tunamshukuru sana Mh. Raisi Mstaafu na Mama Salma Kikwete kwa mchango wao wa mifuko 300 ya Cement itakayofanikisha umaliziaji wa jengo la Zahanati ya Kijiji cha Kwakonje na Nyumba ya walimu",amesema Ridhiwani.
Kwa upande mwingine, Mzee Kikwete tokea amalize muda wake wa kuongoza madarakani amekuwa akiendesha maisha yake kutumia kilimo pamoja na ufugaji wa mifugo mbalimbali.

No comments