Header Ads

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametimiza ahadi


Image result for MAKONDA


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametimiza ahadi ya kugharimia matibabu Ahmed Albaity aliyevunjika uti wa mgongo baada ya kuanguka wakati akiogelea takribani miaka 10.
Albaity alivunjika uti wa mgongo mkoani Tanga alipokuwa akiwafundisha wenzake kuogelea, lakini alianguka na kuvunjika uti wa mgongo. Makonda alitoa ahadi ya kumsaidia Albaity wakati wa shughuli ya upimaji afya bure uliofanyika kwa siku tano katika Meli ya Jeshi la China, mwishoni mwa mwaka jana. Kijana huyo aligundulika kuwa anahitaji matibabu maalumu yanayopatikana nchini China.
Baada ya taarifa kutoka kwa madaktari hao Makonda aliamua kumsaidia kwa kumgharamia safari yake pamoja na matibabu kwa kuwa kijana huyo alishindwa kugharamia matibabu hayo kwa kuwa sindano moja anayotakiwa kuchomwa inagharimu Sh milioni 52. Makonda amemkabidhi tiketi ya ndege pamoja na tiketi tatu kwa ajili ya atakaokuwa nao kumsaidia kwenye matibabu katika Hospitali ya Beijing Puhua International pamoja na fedha kwa ajili ya matibabu na malazi.
Alisema gharama ya matibabu ni zaidi ya Sh milioni 100. Mkuu wa Mkoa aliwashukuru wote walioguswa na kumuunga mkono kufanikisha safari ya matibabu kijana huyo. “Nawaomba wananchi wangu wa dini zote kumuombea kijana huyu ili aweze kupona na kurejea katika hali yake ya kawaida na aweze kuendelea na shughuli za kulijenga taifa,” alisema Makonda. Albaity alisema ameishi kwa mateso muda mrefu kutokana na kukosa uwezo wa kumudu gharama za matibabu na amekuwa akiomba watu wamsaidie, lakini wengi wao wamekuwa wakimvunja moyo kwa kumwambia hawezi kupona. Aliwaomba Watanzania kumuombea ili arejee akiwa mzima.

No comments