Header Ads

UFAHAM UGONJWA WA MSHIPA WA NGIRI (HERNIA/HYDROCELE)

UFAHAM UGONJWA WA MSHIPA WA NGIRI (HERNIA/HYDROCELE) 

Image result for UGONJWA WA NGIRI




Ngiri au Hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo fulani mwilini kupoteza uimara wake au kuwa na uwazi na hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo katika sehemu vinapostahili kuwepo. 

Katika mwili wa binadamu, maeneo ambayo tatizo hili hutokea mara kwa mara ni maeneo ya tumboni, katika eneo la kinena, eneo la paja kwa juu na pia ngiri inaweza kutokea katika eneo ambalo mtu alifanyiwa upasuaji. Ugonjwa huu wa ngiri unawapata wanaume na wanawake wa rika zote. 

Mshipa wa ngili ni jina linalokusanya magonjwa kama Ngiri kavu (Hernia), Ngiri maji (Hydrocele) na Ngiri nyinginezo kama vile kuvimba kokwa au mfereji unaopitisha manii unaojulikana kitaalamu kama Epididmorchitis.


Ngiri Kavu (Hernia), aina hii ya ngiri huwapata wanawake na wanaume wote kwa ujumla. Ngiri kavu inapompata Mwanamke huitwa Fermoral Hernia, na pindi inapompata mwanaume inaitwa Scrotal hernia. Kwa maana halisi ya ngiri au mshipa wa ngiri ni hali inayotokea katika mwili wa binadamu ambapo sehemu fulani ya nyama ya viungo mbalimbali vya mwili hujipenyeza kupitia sehemu dhaifu ya mwili na kutokeza upande wa pili.

Sehemu hiyo inayoathiriwa mara nyingi huwa ni maeneo ya tumbo, kokwa, pumbu na kadhalika ambapo baadhi ya viungo vya mwili vilivyomo tumboni hujipenyeza kupitia vitundu vinavopitisha mishipa ya fahamu inayohudumia kokwa (Spesmatic Cord), hivyo baada ya kujipenyeza huteremka hadi ndani ya korodani hali ambayo hukamilisha kuwepo kwa ugonjwa wa mshipa wa ngiri.

Pamoja na hivyo mshipa wa ngili hujitokeza sehemu mbalimbali za mwili na hupewa majina tofauti kutokana na sehemu ulipojitokeza, kwa mfano ngiri ya tumbo inajulikana kitaalamu kama Abdominal Hernia, pia watoto wanaozaliwa na vitovu vikubwa inaitwa Umbilical Hernia, na pale ngiri inapojitokeza katika sehemu ya haja kubwa inaitwa Anal Herni. Dalili zake hazitofautiani sana hata hivyo ngiri hujitokeza bila maumivu yoyote isipokuwa kuna baadhi ya ngili hujitokeza na maumivu makali hutegemea ngiri ilivotokeza. 

Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa wa mwili wa kupitiliza au kuongezeka uzito kwa ghafla, pia kua na kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua.
Mojawapo ya dalili za ugojwa wa ngiri ni pamoja na; 
• Uvimbe unaoteremka kuingia ndani ya korodani unaojulikana kitaalamu kama Direct Scoratal inguinal Hernia.
• Uvimbe unaojitokeza tumboni na kuteremka hadi ndani ya korodani, uvimbe huu hauumi na unaweza kurudishwa kwa urahisi iwapo mgonjwa atalala chali na kusukuma kwa vidole, uvimbe huu. 

• Na pindi ukikubali kurudi ndani ndipo unapoitwa Reduible direct scrotal inguinal hernia. 

• Na pia endapo utashindikana kurudi tumboni ndipo unapoitwa Irreduible direct scrotal inguinal hernia.

Ugojwa huu wa ngiri unaweza kutibika kwa kupitia dawa asilia ukiacha uperesheni iwapo mgonjwa atazigundua dalili zake mapema na kufika katika zahanati yetu ya Nsong’wa Traditional Clinic kumuona Dr. Damaki, ili uweze kupata dawa itakayotibu na kumaliza kabisa maradhi ya Ngiri na kusababisha uweze kupona tatizo hili kwa mda mfupi kabisa.
Image result for UGONJWA WA NGIRI


DOCTOR SYLAS

No comments