Header Ads

TMA yatoa tahadhari

Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini 
Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa hali mbaya ya hewa katika maeneo 
yote ya pwani kuanzia leo usiku.


Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo (Jumapili) na kudai kutakuwepo vipindi vifupi vya mvua kubwa ambazo zinatarajiwa kunyesha katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Mara, Simiyu, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Morogoro, Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya unguja na Pemba.
Mbali na hilo, TMA imesema kutakuwepo upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayozidi mita 2 ambavyo vinatarajiwa katika ukanda wote wa Pwani
Kwa taarifa kamili angalia hapa chini

No comments