Header Ads

tetesi ya soka barani ulaya

Huddersfield Town yajihakishia kusalia ligi ya England

Laurent Depoitre mfungaji wa bao lililowahakisha Huddersfield kusalia ligi kuu ya nchini England

Huddersfield Town wamejihakishia nafasi ya kusalia katika ligi hiyo kwa msimu ujao baada ya kwenda Sare ya kufungana goli 1-1 na Chelsea.
Kwa matokeo hayo ya Huddersfield, Swansea City inakuwa timu ya tatu kushuka daraja na kuunga na Stoke city na West bromwich Albion.
Na matokeo hayo yanaifanya Chelsea kuwa katika wakati ngumu kufuzu kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya.
Leicester City ikicheza nyumbani katika dimba la King Power waliwatungua Arsenal kwa magoli 3-1.
Manchester City wamezidi kuwa na msimu bora baada ya kuichapa Brighton kwa magoli 3-1 na kuweka rekodi ya timu iliyopata alama nyingi zaidi kwa msimu na timu iliyofunga magoli mengi zaidi kwa msimu wakiwa na magoli 105.
Tottenham hotspurs imejihakishia nafasi ya kucheza michezo ya klabu bingwa ulaya kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Newcastle United.
Leo unapigwa mchezo mmoja wa ligi hiyo Wagonga nyundo West Ham watakuwa wenyeji wa Mashetani Wekundu Man United

Barcelona yawika huku Real Madrid ikilazwa

Dembele akifunga mojawapo ya mabao yake mawili katika mechi dhidi ya Villareal ambayo Barcelona ilipata ushindi wa 5-1
Barcelona imesalia na mechi mbili kuandikisha rekodi ya kutofungwa msimu mzima katika ligi ya La Lga baada ya kuicharaza Villarreal huku Ousmane Dembele akifunga mabao mawili.
Philippe Coutinho alifungua mfereji wa mabao baada ya kipa kupangua shambulio la Dembele huku Paulinho akifunga bao la pili.
Wakati huohuo nahodha wa Real Madrid Sergio Ramos alikosa mkwaju wa penalti ,akajifunga goli moja kabla ya kufunga mkwaju mwengine wa penalti huku Real Madrid ikipoteza kwa Sevilla 3-1.
Wissam Ben Yader aliiweka mbele Sevilla kabla ya Steven Nzonzi kufunga bao la pili kufuatia pasi ya Miguel Layun.

Sergio Ramos amejifunga bao mawili yote dhidi ya SevillaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionSergio Ramos amejifunga bao mawili yote dhidi ya Sevilla

Ramos alijifunga kufuatia krosi iliopigwa na Gabriel Mercado na hivyobasi kuipatia Sevilla uongozi wa 3-0. Real ilijipatia bao la kufutia machozi kupitia Borja Mayoral aliyefunga kichwa kabla ya Ramos kufunga mkwaju wa penalti na kuipatia Real 2.
Real ambao walicheza bila nyota wao Cristiano Ronaldo itakabiliana na Liverpool mjini Kiev Mei 26.
Tukirudi katika uwanja wa Nou Camp, Lionel Messi alifunga pasi nzuri kutoka kwa Andres Iniesta.
Nicola Sansone aliisawazishia Villareal kabla ya Dembele kufunga mabao mawili mwisho wa kipindi cha pili.
Dembele alicheka na goli lililokuwa wazi kufuatia kazi nzuri ya Ivan Rakitic kabla ya kufunga bao lake la pili baada ya kupokea mpira kutoka nusu ya uwanja akawachenga mabeki kadhaa na kumpiga kanzu kipa Sergio Asenjo.
Iniesta alipatiwa heshima ya hali ya juu alipokuwa akitoka uwanjani muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza .
Nahodha huyo wa Barcelona anaondoka katika klabu hiyo ambapo amecheza kipindi chote cha maisha yake ijapokuwa kuna ripti kwamba huenda anaelekea nchini China.


No comments