Header Ads

asa Vanessa Mdeena Juma Jux wanaikata kiu yako uliyoitunza kwa muda mrefu

Sahau na achana na yale maneno yalizagaa mtandaoni kwamba wawili hawa hawapikiki chungu kimoja baada ya V-Money kuhusishwa na msanii mmoja wa Kimataifa.


Image result for PICHA YA JUX


Sasa Vanessa Mdeena Juma Jux wanaikata kiu yako uliyoitunza kwa muda mrefu ya wao kuachia ngoma pamoja. Ngoma hii ambayo inasemekana itabamba mawimbi ya radio na mashabiki inakwenda kwa jina la “Juu” na imeachiwa kwa mara ya kwanza hii leo Mkitoni ikipitia mikono yaLufa- Switch Records.

Huu umekuwa mwaka mzuri kwa wawili hawa ambao wamepiga tour za kutosha nchini kwenye msimu wa Fiesta huku wimbo “Wivu” wa Jux ukiendelea kusumbua kwenye chati mbalimbali zamuziki.
Vanessa anatuwakilisha Watanzania kwenye msimu mpyawa Coke Studio Africa unaoanza Jumamosi hii huku pia akiwa mmojawapo wa wasanii wa nyumbani wanaochuana kuwania tuzo za MTV Base MAMAs kwenyekipengele cha msanii bora wa kike.
Kama hiyohaitoshi Vanessa Mdee atakinukisha wikiendi hii mjini Mombasa akiwa na wakali kama Wizkid na Chris Brown.


No comments