Header Ads

Marekani imeionya Ethiopia kutotumia vibaya hali ya tahadhari iliyoidhinishwa Jumapili nchini.

Waandamanaji wa kabila la Oroma wamekuwa wakitaka haki zaidi kisiasa na kiuchumi
Marekani imeionya Ethiopia kutotumia vibaya hali ya tahadhari iliyoidhinishwa Jumapili nchini.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje amesema ni lazima serikali ya Ethiopia ifafanue vipi inavyonuia kuhakikisha kuwa haki za raia zinadumishwa wakati wa miezi hiyo 6 ambapo hali hiyo ya tahadhari imeidhinishwa.

Jumanne, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameiomba serikali iwaruhusu raia haki yao kulalamika.
Marekani ndio nchi ya hivi karibuni kuelezea wasiwasi kuhusu hali ya tahadhari iliyoidhinishwa Ethiopia.

Imeidhinishwa baada ya ghasia za miezi kadhaa za kuipinga serikali katika maandamano ya makabila mawili kubwa nchini humo.
Msemaji huyo wa Marekani ameonya kuwa kunyamazisha wakosoaji serikali kutaizidisha hali kuwa mbaya zaidi.

Jeshi limetawanywa na mikusnayiko ya umma yamepigwa marufuku kama sehemu ya hali hiyo ya tahadhari.

Mamia ya watu wamefariki tangu kuzuka maandamano hayo Novemba mwaka jana, na serikali imekiri kuwa huedna idadi hiyo ikawa ni karibu watu 500

No comments