Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameagiza viongozi wote wa Serikali walioalikwa kuhudhuria sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kutohudhuria sherehe hizo.
Rais wa Tanzania
Dkt. John Magufuli ameagiza viongozi wote wa Serikali walioalikwa
kuhudhuria sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa
kutohudhuria sherehe hizo.
Ameagiza wale ambao walishalipwa fedha ya posho na safari kwa ajili hiyo wazirejeshe.
Sherehe
hzo zimepangiwa kufanyika tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Wilaya ya
Bariadi Mkoani Simiyu, kaskazini magharibi mwa Tanzania.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema kupitia taarifa kwamba Rais
Magufuli ametoa maagizo hayo ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya
awamu ya tano ya kubana matumizi yasiyo ya lazima na kuelekeza
rasilimali nyingi katika shughuli za maendeleo ya nchi.
Viongozi
waliotakiwa kufuta safari zao za kwenda Bariadi ni pamoja na Wakuu wote
wa Mikoa, Wakuu wote wa Wilaya, Wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali
za Mitaa, Mameya na Wenyeviti wote wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,
Miji na Wilaya pamoja na watumishi ambao huambatana nao wakiwemo
madereva na wasaidizi wao.
Inakadiriwa kwamba idadi ya waliotakiwa kufuta safari ni takriban 1,500.
Viongozi
wote wa Mikoa na Wilaya watekakiwa kubaki katika maeneo yao ya kazi na
kujiwekea utaratibu wa jinsi ya kuienzi siku ya Kumbukumbu ya Muasisi wa
Taifa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
aliyefariki dunia miaka 17 iliyopita.
Post a Comment