Header Ads

Watu wanaoshukiwa kuwa ni waasi wa kundi la wanamgambo la Al-Shabab, wameuwa watu sita kwenye shambulio la kaskazini mashariki kwa Kenya.

Watu wanaoshukiwa kuwa ni waasi wa kundi la wanamgambo la Al-Shabab, wameuwa watu sita kwenye shambulio la kaskazini mashariki kwa Kenya.

image-resizer

image-resizer
Ali Roba, gavana wa kaunti ya Mandera amesema mtu mmoja pia amejeruhiwa kwenye shambulio hilo. Walinzi walifanikiwa kuwaokoa watu 27 waliokuwepo kwenye eneo hilo.
Kundi la Al-Shabab linapambana na serikali ya Somalia inayosaidia na Umoja wa Mataifa na wamewahi kufanya mashambulio mengi kwa jirani zao, Kenya.
Wanamgambo hao wamelilenga mara nyingi eneo la Mandera linalopakana na Somalia. Huwalenga watu wasiotoka katika eneo hilo pamoja na wanajeshi.

No comments