Baraza la vijana wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema la toa msaada wa chakula
Baraza la vijana wa chama
cha Demokrasia na maendeleo Chadema-BAVICHA tawi la mulepa kata ya ndala Katika
manispaa ya Shinyanga limetoa msaada wa vyakula na mavazi kwa watoto wenye
ulemavu wanaolelewa katika kituo cha BuhangijaJumuishi,ilikupunguza changamoto
zinazowakabili.
Msaada uoliotolewa na baraza
hilo la vijana wa chama cha Demokrasia na Maendeleo chadema,ni Pamoja na mchele,mafuta ya kupikia sabuni,vifaa vya
kufanyia usafi,nguo na viatu vyote vikiwa na thamani ya shilingi Laki mbili
Akizungumza mara baada ya
kukabidhi msaada huo kwa mlezi wa kituo hicho,mwenyekiti wa BAVICHA tawi la
Mlepa kata ya Ndala bwana AFRED MASANJA amesema vijana hao wameguswa na kuona
umuhimu wa kusaidia kituo hicho ambacho kina upungufu wamahitaji.
Mmoja wa wajumbe wa serikali
ya mtaa wa Mulepa, bwana JOHN ROBERT
ameahidi kuendelea kusaidia na kushirikiana na kituo hicho kwa hali na mali ili kusababisha chakula hakikose kani shuleni hapo
Kwa upande wake mlezi wa
kituo hicho bwana STANLEY WAGALA amewashukuru baraza la vijana wa chama cha
Demokrasia na maendeleo akisema waendelee kujitolea ili kusaidia watotohao.
KITUO
CHA BUHANGIJA Jumuishi kilichopo katika manispaa ya Shinyanga kinalea watoto
wenye ulemavu mbali mbali wakiwemo wenye albinism,wasioona,na viziwi.
Post a Comment