Nigeria wakamata gunia 102 za ‘mchele wa plastiki’
Sakata la ‘mchele wa plastiki’ bado linaendelea kushika kasi katika
nchi mbalimbali za Afrika baada ya Tanzania hivi karibuni kukanusha
kuwepo kwa mchele huo.
Huko nchini Nigeria maafisa wa nchi hiyo
wamekamata magunia 102 ya ‘mchele wa plastiki’ yaliyokuwa yanaingizwa
nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu
huu wa sherehe, kulingana na afisa wa forodha katika mji mkuu wa nchi
hiyo , Lagos.
Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa “plastiki”
,baada ya kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida
na ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na
binadamu “, Haruna Mamudu aliongeza katika kauli yake juu ya tukio hilo.
Aliwawaonya wahujumu wa uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha
sherehe kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na
mkono wa sheria.
Bwana Mamudu hakuelezea ni vipi mchele huo wa plastiki ulitengenezwa lakini ulikua na nembo iliyoandikwa “Best Tomato Rice”.
Uchunguzi unaendelea kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa
kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia
wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo
haramu mbele ya sheria”.
Nchini Uchina, kuliwahi kuwa na sakata ya chakula mwaka jana baada ya
kubainika kuwa kuwepo kwa mchele uliotengenezwa kwa plastic.
Nchini Tanzania Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), iliwatoa
hofu Watanzania kuhusu taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii
kuwa kuna mchele unaotengenezwa kwa plastiki kutoka nchini China.
Post a Comment