wasichana wawili wamelipua mabomu mawili nchini Nigeria
wasichana wawili wamelipua mabomu mawili katika soko lililoko kwenye
jimbo la Borno na kumuua nchini Nigeria takriban mtu mmoja.
Mwanamgambo mmoja
katika mji wa Maiduguri amesema kuwa watoto wasichana hao ambao pia
waliuawa walikuwa na umri wa miaka saba na minane.
Alisema kuwa
aliwaona wakitoka nje ya Bajaji na kujaribu kuzungumza na mmoja wao,
ambaye baadae alielekea kwenye jengo lenye maduka mengi na kulipua
vilipuzi.
Hakuna aliedai kuhusika na shambulio hilo, lakini
waandishi wa BBC wanasema kundi la Boko Haram mara kwa mara hutumia
wanawake na watoto katika mashambulio yake ya mabomu.
Post a Comment