MSAADA UMETOLEWA KWA WAZEE NA VIJANA WASIOJIWEZA KOLANDOTO MKOANI SHINYANGA
Jamii
imeombwa kuwa na moyo wa kuwasaidia wazee wasiojiweza wanaoishi katika kituo
cha KOLANDOTO kilichopo katika manispaa ya Shinyanga ambao wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali ikiwemo upungufu wa mahitaji muhimu.
Akikabidhi
msaada wa vitu mbalimbali kituoni hapo, mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana
na rushwa TAKUKURU katika mkoa wa Shinyanga Bw. AMOSI GASTO MKONO amewaomba
wananchi wa Shinyanga kuendelea kuwasaidia wazee hao ambao wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa chakula na uchakavu wa majengo
wanayoishi.
Mkuu huyo wa
TAKUKURU pia ameahidi kumsomesha mtoto mmoja miongoni mwa watoto wanne
waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka kesho 2017,ambao wazazi wao
walikuwa wanaishi katika kituo hicho na baadaye kufariki dunia.
Naye afisa mfawidhi
wa kituo hicho Bi. SOFIA KANG’OMBE amesema licha ya kituo hicho kukabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu mkubwa wa chakula na mavazi ,majengo wanayoishi
wazee hao ambayo yalijengwa tangu mwaka
1984 mpaka sasa bado hayajakarabatiwa hali iliyosababisha yawe na nyufa na
kutishia usalama wa wazee hao.
Badhi ya misaada
ambavyo imetolewa na TAKUKURU mkoa wa Shinyanga katika kituo hicho ni pamoja na
vyakula,nguo na sabuni ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha siku ya
maadili nchini Tanzania.
ANGALIA VIDEO YA MAAZIMISHO 55 YA UHURU
Post a Comment