Header Ads

Polisi nchini Uholanzi wamemkamata kijana wa miaka 30



Image result for picha ya Polisi nchini Uholanzi
Polisi nchini Uholanzi wamemkamata kijana wa miaka 30 anayetuhumiwa kupanga kufanya shambulio la kigaidi.

 Polisi wamesema wamekuta bunduki ya aina ya Kalashnikov AK-47 iliyokuwa imejaa risasi, katika nyumba ya mtuhumiwa huyo mjini Rotterdam, pamoja na milipuko mingine kadhaa. 


Aidha polisi wamesema walianza msako huo baada ya kupokea taarifa za kijasusi Jumatano iliyopita. Mashirika ya kijasusi ya barani Ulaya yameonya kwamba kundi linalojiita "Dola la Kiislam" linaweza kufanya shambulio katika kipindi cha sherehe za Krismasi.

No comments