Shule ya Msingi Old Shinyanga ya kabiliwa na upungufu wa walim
Wanafunzi wa Shule
ya Msingi Old Shinyanga iliyopo katika
kata ya Old Shinyanga wameiomba serikali kuwawekea mazingira wezeshi yatakayosaidia kuinua kiwango cha
Elimu
Wanafunzi hao
wamesema kuwa kushuka kwa kiwango cha Elimu shuleni hapo inasababishwa na
ukosefu wa baadhi ya mahitaji ya msingi ikiwemo upungufu walimu vifaa vya kufundishia
Kwa upande wake
Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule ya msingi Old Shinyanga, METHOD MZINGO amekiri kushuka kwa kiwango cha ufaulu ikilinganishwa
na miaka minne ya nyuma,ambapo ameiomba serikali kushughulikia tatizo la
upungufu wa Walimu.
Amewaomba wazazi
na walezi kushirikiana na walimu kufuatilia mwenendo na maendeleo ya watoto wao
ili kuwawekea msingi thabiti kielimu.
Shule ya msingi
Old shinyanga iliyopo katika manispaa ya
Shinyanga imeshika nafasi ya 29 kati ya shule 52,ikilinganishwa na mwaka 2014
ambapo ilishika nafasi ya 14 kati ya shule 52 za manispaa ya Shinyanga.
Post a Comment