watu 30 wamekufa mara baada ya boti kuzama kwenye maji
Polisi nchini Uganda wanasema takriban watu 30 wamekufa maji baada ya boti yao kuzama katika ziwa Albert magharibi mwa taifa hilo.
Abiria wengi walikuwa wanasoka na mashabiki wao waliokuwa wakielekea katika mechi ya kirafiki ya kuadhimisha siku ya Krismasi.
Mafisa wa polisi wanasema chombo hicho kilikuwa kimejaa kupitia kiasi huku abiria wakiimba a kupiga tarumbeta.
Boti hiyo inadaiwa kuzama katika maji yaliotulia .
Ajali hutokea mara kwa mara katika ziwa Albert ,ambapo maboti hujaa kupitia kiasi licha ya kutofanyiwa ukarabati wowote.
Post a Comment