WATAO HUJUM TASAF KUCHUKULIWA HATUA
Walengwa wa TASAF awamu ya tatu Mpango wa kunusuru
kaya masikini mkoa wa Shinyanga wameombwa kutoa taarifa dhidi ya watendaji
watakaohusika kufanya hujuma hasa vitendo vya rushwa,katika utekelezaji wa
mpango huo
Mratibu wa TASAF Mkoa wa Shinyanga bwana Dotto Maligisa amewaomba walengwa
kutoa taarifa Pale watakapobaini kuwepo udanganyifu wowote utakaofanywa na
watendaji zikiwemo kamati za usimamizi ngazi ya serikari ya mtaa,kitongoji na
kijiji,ikiwemo mianya ya rushwa.
Hatua hiyo ni kufuatia tetesi kutoka kwa baadhi ya
wananchi kwamba baadhi ya watendaji hutumia fursa hiyo kuwashawishi walengwa
kugawana nao Pesa wanazopokea kwenye mpango huo.
Mratibu huyo wa TASAF Mkoa wa Shinyanga amesema tayari
Mkoa wa Shinyanga umefanikiwa kuwafikia walengwa 34,883 kati ya 45,000
waliokuwa wametarajiwa.
Aidha amesema kati ya walengwa hao 641 wameondolewa
kwenye mpango kutokana na kukosa sifa.
Asema
TASAF awamu ya tatu mpango wa kunusuru kaya masikini umeleta matokeo cmehanya
baada ya walengwa wengi kujikwamua kiuchumi katika maeneo ya kilimo,ufugaji na
ujenzi
Post a Comment