VIDEO: Rais Magufuli kwenye sherehe za Uhuru DSM
Leo December 9 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli alikuwa mgeni Rasmi kwenye sherehe za maadhimisho ya uhuru wa Tanzania bara katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam, kama unakumbuka mwaka jana Sherehe hizo hazikufanyika na badala yake Rais Magufuli aliagiza kufanya usafi na fedha iliyokuwa imepangwa ilielekezwa kwenye upanuzi wa barabara ya Mwenge.
Ikiwa ni mara ya kwanza kwa sherehe hizo kufanyika chini ya uongozi wa Rais Magufuli, leo kwenye sherehe hizo Rais Magufuli alipata nafasi ya kuhutubia ambapo amesema…..
>>>’Sherehe za miaka 55 nimeamua zifanyike kwa sababu gharama zake ni ndogo sana, kwanza hakuna hata chakula baada ya sherehe hii, hakuna dhifa ya Taifa, tukishamaliza hapa tumemalizana’-Rais Magufuli
>>>’Nimeamua sherehe hizi zifanyika hapa Dar es salaam kwa sababu ninaamini hii itakuwa sherehe ya mwisho kufanyika hapa Dar es salaam, ni matumaini yangu sherhe ya mwaka kesho itafanyika makao makuu ya nchi ambayo ni Dodoma’-Rais Magufuli
VIDEO: Rais Magufuli alivyoonyesha ukakamavu baada ya kukagua gwaride,Bonyeza play hapa chini kutazama
VIDEO: Kwata ya kimya kimya wakionyesha uwezo wao kwenye sherehe za Uhuru DSM, Bonyeza play hapa chini Kutazama
Post a Comment