facebook kuboreshwa zaidi
Kampuni ya mtandao wa Facebook imesema kuwa wameanzisha
upelelezi ili kubaini akaunti feki zilizoanzishwa na watumiaji kupitia
mtandao huo.
Tayari imeshaanza kuwatumia wafanyakazi kutoka nje ya kampuni hiyo
watakaoweza kugundua kompyuta zinazotumika mara kwa mara ambazo
zinahusiana na akaunti hizo feki. Mara kadhaa kampuni hiyo imekuwa
ikilalamikiwa na watumiaji wa mtandao huo kushindwa kuchukua hatua juu
ya wale wanaotoa taarifa feki kwa kutumia akaunti hizo.
Inadaiwa kuwa baadhi ya watu hutumia akaunti hizo feki walizofungua
kupitia mtandao huo kwa ajili ya kuweka habari ili wapate watazamaji
wengi ili kuzidi kujipatia fedha nyingi.
Post a Comment