watu 12 wamefariki dunia baada ya lori kuacha njia
Wakati wakristo kote Duniani wakijiandaa na sikukuu ya Krisimasi, huko nchini Ujerumani watu 12 wamefariki dunia baada ya lori kuacha njia na kuelekea katika soko maarufu kwa maandalizi ya Krisimasi katikati ya mji wa Berlin.
Taarifa za awali za serikali ya Ujerumani zimeeleza kuwa tukio hilo ni la makusudi.
Pamoja na kusababisha vifo vya watu tisa,lakini Lori hilo pia limejeruhi watu 50 baada ya kuingia katika soko hilo lenye mkusanyiko mkubwa wa watu.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere, amesema kuna kila dalili kwamba tukio hilo huenda ni la kupangwa na kwamba Polisi wanaendelea na uchunguzi.
Hata hivyo Polisi wamesema kuwa wanachunguza kufuatia gari lililosababisha maafa hayo kudaiwa kuwa lilikuwa na namba za usajili za polisi na kwamba lilibiwa katika jengo ambalo kulikuwa na kazi ya ujnezi huko Poland.
Msemaji wa idara ya zima moto mjini Berlin, Sven Gerling, amesema walishtushwa na kile walicho kiona katika eneo la tukio
Nao Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa waliliona lori hilo likielekea katika viunga vya soko hilo kwa kasi karibu na kanisa la kumbukumbu ya Kaisari Wilhelmo.
Polisi wamefanikiwa kumkamata mtu wanayedhani alikuwa akiendesha gari hilo ambapo abiria aliyekuwa ndani ya gari hilo na ambaye hajafahamika mara moja alikufa katika ajali hiyo.
Post a Comment