Rais wa Tanzania John Magufuli ametangaza kwamba taifa hilo litanunua ndege zaidi katika juhudi za kufufua shirika la ndege
Rais wa Tanzania
John Magufuli ametangaza kwamba taifa hilo litanunua ndege zaidi katika
juhudi za kufufua shirika la ndege la taifa hilo.
Amesema serikali
yake imedhamiria kununua ndege nne zikiwemo ndege kubwa tatu ambazo
zitasaidia kuinua "uchumi wa nchi kwa kuwezesha watalii kuja hapa nchini
moja kwa moja kutoka nchi zao."
Dkt Magufuli alisema hayo baada
ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Masoko ya Afrika wa
Kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Boeing yenye makao yake nchini
Marekani Bw. Jim Deboo katika ikulu jijini Dar es Salaam.
Amesema
Tanzania inpanga kununua ndege aina ya Boeing 787 Dash 8 Dreamliner
yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini
humo Juni 2018.
Ndege nyingine ambazo Tanzania itazinunua ni ndege
moja aina Bombardier Q400 Dash 8 NextGen inayotarajiwa kuwasili Mwezi
Juni 2017, ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati
ya abiria 137 na 150 na zinazotarajiwa kuwasili nchini kati ya Mei na
Juni, 2018.
chanzo bbc
Post a Comment