VIDEO: Kwata ya kimya kimya JWTZ
December 9 2016 zimefanyika sherehe za maadhimisho ya 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru Dar es salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alikuwa mgeni Rasmi.
Moja ya vitu vilivyopamba sherehe hizo ni pamoja na kwata ya kimya kimya, kwata hiyo ya kimya kimya imefanywa na kundi ambalo imeelezwa limeundwa mwezi April 2016 na kwenye sherehe za Uhuru hili ni onyesho lao la tatu.
Askari hao wameonyesha namna ya kuchezea silaha jinsi watakavyo na jinsi ambavyo wanaweza kufanya vitendo kwa haraka zaidi na kwa usahihi, kingine ni kuwa askari hao wote wana kilo si zaidi ya 45. Bonyeza play hapa chini kutazama.
VIDEO: Rais Magufuli alivyoonyesha ukakamavu baada ya kukagua gwaride, Bonyeza play hapa chini kutazama
Post a Comment