chadema mkoani tabora kuwasimamisha kazi
Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani TABORA
kimewasimamisha kazi kwa muda usiojulikana viongozi wake wawili wa ngazi ya
wilaya ambao ni mwenyekiti wa wilaya ya Igunga
JOSEPH KASHINDYE na katibu wake IDDY ATHUMANI .
Katibu wa chadema mkoa wa Tabora ALLY MWAKILIMA amesema viongozi hao
wamesimamishwa uongozi tangu tarehe 30 mwezi uliopita baada ya kukiuka
katiba ya chama hicho.
Viongozi waliosimamishwa ni mwenyekiti JOSEPH KASHINDYE na
katibu wake IDDY ATHUMANI wamekiri kupokea barua ya kusimamishwa uongozi tangu
tarehe 3 mwezi huu ameeleza kuwa maamuzi
ya kuwasimamisha yametolewa na
baraza la uongozi la Mkoa kupitia chama
hicho baada ya viongozi hao wawili kudaiwa kukiuka na kuvunja katiba ya chama
Mwezi ulipita viongozi hao wawili walisimama mbele ya
mahakama ya wilaya iliopo mkoani TABORA
kutoa ushaahidi kwa upande wa mtu
alieshitaki chama huku huku wakiwa
wanajua wazi kuwa nikinume na katiba ya chama hicho.
Amebainisha kuwa pamoja na
kuwasimamisha viongozi hao pia baraza la chama limemuagiza katibu wa wa
chama hicho IDDY ATHUMANI kukabidhi mali zote za chama kwa katibu wa jimbo la
Igunga mbele ya mwenyekiti wake ikiwa ni pamoja na kujieleza ndani ya siku nne
Post a Comment